Alikiba amekanusha taarifa zilizoenea kuwa atatumbuiza kwenye shindano
la Miss Tanzania 2016 litakalofanyika Jumamosi hii mjini Mwanza.
Taarifa
hizo zilizosambaa zimedai kuwa Alikiba na Christian Bella ndio wasanii
watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo lakini Kupitia mtandao wa Instagram,
hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Aje’ ameandika, “Taarifa Muhimu : Napenda
Kuwajulisha Ya Kuwa Sitakuwepo.”
Tamasha hilo litakuwa likifanyika
mkoani humo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo nchini.
No comments:
Post a Comment