Ndege hiyo iliteleza na kuvuka barabara inayotumiwa na ndege
kupaa na kutua katika uwanja wa LaGuardia jijini New York.
Gavana huyo wa Indiana amewaambia wanahabari kwamba yuko salama
baada ya kisa hicho.
Hakuna aliyejeruhiwa.
Bw Pence na abiria wengine takriban 30 waliokolewa kupitia
mlango wa dharura wa ndege upande wa nyuma.
Alikuwa anatoka mkutano wa kampeni Fort Dodge, Iowa.
Uwanja wa ndege wa LaGuardia kwa muda usiojulikana, maafisa
wamesema.
Rubani anadaiwa kukanyaga breki na abiria wanasema walinusa
harufu ya raba ikiungua.
Kanda za video za runinga zimemuonesha Bw Pence baadaye
akiwa amesimama kwenye mvua karbu na magari ya huduma za dharura, akizungumza
na baadhi ya maafisa.
Baadaye aliandika kwenye Twitter:
"Nashukuru sana kwamba kila mtu aliyekuwa kwenye ndege yetu yuko salama.
Nashukuru maafisa wa dharura na wote waliotuombea. Tutarejea kwenye kampeni
kesho!"
Amesema matope yaliruka na kujaa kwenye kioo cha sehemu
ya mbele ya ndege.
Mgombea urais wa chama cha
Republican Donald Trump alimpigia simu Bw Pence kumjulia hali baada ya kisa
hicho, maafisa wa kampeni wamesema.
Msemaji wa Trumo Stephanie Grisham alisema mgombea huyo
alikuwa kwenye msafara wa kampeni akielekea Geneva, Ohio.
Bw Trump alizungumzia ajali hiyo
kwenye mkutano wake wa kampeni baadaye akisema: "Mnajua, kulitokea ajali
kubwa ya ndege.
"Ndege imeteleza kutoka
barabara uwanja wa ndege na ilikaribia sana kuwa mbaya, kuwa mbaya sana,
nimezungumza na Mike sasa hivi na yuko salama. Alitoka. Kila mtu yuko
salama." Bw Pence aliahirisha hafla ya kuchangisha pesa ambayo ilifaa
kuandaliwa katika jumba la Trump Tower eneo la Manhattan, na akaelekea moja kwa
moja hadi hotelini.
Haijakuwa wiki njema kwa gavana
huyo wa Indiana.
Jumatano, alitangaza kwenye Twitter
kwamba mbwa wake kwa jina Maverick, alikuwa amefariki akiwa na miaka 13.
No comments:
Post a Comment