Rais huyo, alliyemwita Rais Barack Obama "mwana wa
kahaba" na akasema kiongozi huyo anaweza "kwenda jehanamu",
amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupata ufunuo alipokuwa safarini kutoka
Japan.
Amewatusi pia watu wengine mashuhuri. Alimwita kiongozi wa
kanisa Katoliki duniani Papa Francis "mwana wa kahaba" (Ufilipino ni
taifa lenye Wakatoliki wengi).
Amewahi kumtusi pia waziri wa mambo ya nje wa Marekani John
Kerry kwa kumuita "mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa
Marekani nchini Ufilipino kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa
kahaba".
Bw Duterte amesema kuwa alipokuwa kwenye ndege, na watu wengine
wote walikuwa wamelala, alisikia sauti ikimuonya: usipokoma, nitaiangusha ndege
hii.
Amesema sauti hiyo ilijitambulisha kuwa ilitoka kwa Mungu.
Amewaahidi watu waliokusanyika mji wake wa nyumbani wa Davao
kwamba ahadi kwa Mungu ni sawa na ahadi kwa Wafilipino.
Rais Duterte ni kiongozi ambaye msimamo wake na matamshi yake
huzua utata mara kwa mara.
Amesomea taaluma ya sheria na alipanda cheo hadi kuwa mwendesha
mashtaka kabla ya kuteuliwa kuwa naibu meya wa Davao wakati wa mapinduzi
yaliyomuondoa madarakani Ferdinand Marcos mwaka 1986.
Alikuwa meya mwaka 1988 na kushikilia wadhfa huo kwa kipindi cha
miaka 10, kabla ya kushinda kiti cha ubunge katika Bunge la Congress halafu
akarejea kwenye kiti cha umeya mwaka 2001.
Alijijengea umaarufu kwa kupiga vita baadhi ya matatizo makubwa
yanayowakabili Wafilipino - uhalifu, makundi ya uasi, na ufisadi. Yote haya
yalipungua kwa kiwango kikubwa wakati alipokuwa kiongozi wa Davao, na kufanya
mji huo kuwa mmoja wa miji salama zaidi nchini Ufilipino.
Duterte ambaye utawala wake ni wa kipekee kwa kuwa
kiongozi mwenye sera za Kijamaa na mwanamageuzi kwa pamoja, sera zake za uchumi
zilikuwa si za kuaminika wakati wa kapeni.
Majuzi, alilinganisha vita vyake
dhidi ya walanguzi wa mihadarati na mauaji ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya
Pili vya Dunia.
Alisema anaweza kuua walanguzi
wengi wa dawa hizo za kulevya sawa na alivyofanya Hitler akiua Wayahudi.
"Hitler aliua Wayahudi milioni
tatu ... kuna waraibu milioni tatu wa dawa za kulevya. Ninaweza kufurahia sana
kuwaua," amesema.
Wayahudi zaidi ya milioni sita
waliuawa na Wanazi chini ya Hitler.
No comments:
Post a Comment