Juan Mata alifunga bao la pekee mechi hiyo baada ya kupata mpira
kutoka kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Paul Pogba alikuwa amegonga mlingoti kwa kombora kali awali na
kusisimua mechi hiyo kipindi cha pili.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kikavu bila upande wowote kupata
kombora la kulenga goli.
Manchester United sasa watakutana na West Ham ambao waliwalaza
Chelsea 2-1.
Ushindi huo wa United ulikuwa wao wa pili katika mechi tano, na
wa nne kwa Jose Mourinho katika mechi 18 alizokutana na Pep Guardiola.
No comments:
Post a Comment