Model Calisah ambaye anadaiwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu amekataa
kuzungumzia mahusiano yake na Wema Sepetu pamoja na kueleza kwanini alisema
hamjui aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother
2014, Idris Sultan.
Wiki
moja iliyopita kupitia kipindi kimoja cha runinga, model huyo alisema hamjui
Idris Sultan.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii,
Calisah alisema ni kweli kwamba hamjui Idris Sultan na wala hakuongea kwa nia
mbaya au kutafuta kiki.
“Mimi nashangaa kwanini watu
wamepanic kisa kusema simjui Idris Sultan, kwani yeye ni nani kila mtu amjue?,”
aliuliza Model huyo. “Wewe kuna wanamichezo wangapi wameshachukua tuzo kubwa
duniani hawajui?. Kwahiyo mimi nadhani watu ambao wananishambulia katika
mitandao hawajui nini wanafanya,”
Aliongeza,”Sikusema hivyo kuonyesha
dharau, kwa sababu nipo karibu na Wema lakini hajawai kuniambia kuhusu mtu kama
huyo na sijawahi kumuona naye, na kama ukiwa na mwanamke halafu akawa
azungumzia mwanaume mwingine hizo ni dharau sana. Kwahiyo kiukweli mimi jamaa
nimeanza kumjua baada ya watu kinitag picha zake katika mitandao ya kijamii,”
Pia model huyo alisema kwa sasa
hawezi kuweka wazi kama ni kweli anatoka kimapenzi na Wema Sepetu huku akidai
Wema ndiye atayekuwa na jibu sahihi juu yake.
No comments:
Post a Comment