Alhamisi hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya msanii wa muziki wa asili
Mrisho Mpoto, ambapo aliitumia siku hiyo kusafiri na kwenda Mkoani Shinyanga
kusherekea siku hiyo na watoto wenye mahitaji maalamu.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Sizonje,
aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainabu Taleck pamoja na wadau
mbalimbali kutembelea kituo hicho.
Kupitia instagram, Mpoto aliandika:
Nawashukuru sana Wadau wote
mlionitakia siku yangu ya kuzaliwa hapo Jana, pia naamini Pendo na Simon wa
Kituo cha Buhangija Shinyanga, watoto wangu niliojitolea kuwalea walifurahi
pia, baada ya kuona nimefunga safari kwaajili yao mpaka shinyanga, pia
nakushukuru Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwa kujitolea muda wako kwaajili watoto
wenye mahitaji maalumu kama Hawa, kweli mh Rais alifanya chaguo sahii kwako!
Bila kuwasahau Wadau wangu wakuu PSPF kwa support yao Kubwa kwa watoto Hawa,
sikua na kikubwa, hicho hicho kidogo tulikula wote Jana! Mwisho kabisa niwaombe
wazazi walikwenda kuwatelekeza watoto pale kituoni nendeni japo wasikie neno
nakupenda tu, wanatamani kusikia hilo neno hawalipati kabisa!!
#hivyondivyoilivyokua
No comments:
Post a Comment