Rais wa Jamhuri ya Muunganowa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali
Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29
Oktoba, 2016.
Jenerali Mstaafu George Marwa
Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.
WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli
amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo Tanzania (TALIRI)
Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza
tarehe 29 Oktoba 2016.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy
Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng'ombe
Makao Makuu ya TALIRI.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais, IKULU
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment