Mkazi wa Machimbo
Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion,
amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya unyang’anyi
wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Mrisho.
Mtuhumiwa wa unyang’anyi wa kutumia silaha na kutoboa macho, Salum Njwete
maarufu ‘Scorpion’ akisindikizwa na polisi na askari magereza kurejeshwa
rumande baada ya kusomewa shitaka lake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar
es Salaam jana.
Scorpion alifikishwa mahakamani
hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore na kusomewa mashitaka na Wakili
wa Serikali, Munde Kalombola.
Akisoma mashitaka hayo, Kalombola alidai
kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli
wilaya ya Ilala.
Munde alidai, Njwele aliiba mkufu
rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili
na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000
mali ya Mrisho.
Kalombola alidai kuwa mshitakiwa
kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani
mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.
Hata hivyo, upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika na upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya
kutaja.
Hakimu Sachore aliahirisha kesi
hiyo hadi Oktoba 19, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Mshitakiwa
alirudishwa rumande kutokana na mashitaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.
No comments:
Post a Comment