Asher Woodworth, kutoka jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika
kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka
kizuizini.
Asher baadaye aliachiliwa huru na polisi.
Aliambia BBC kwamba alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale
alipokabiliwa na maafisa wa polisi.
Yeye ni mwigizaji mjini Portland, Maine.
Anasema: "Nilipata wazo hili nilipokuwa natafakari sana
siku moja."
Anasema alikuwa anataka tu kuwashangaza watu kwa mavazi yake na
kuwafanya "watafakari upya kuhusu matarajio yao".
Alikuwa ametumia matawi ya miti ya aina mbalimbali na anasema
ilimchukua yeye na rafiki yake saa kadha kukamilisha vazi hilo.
Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa
"yananukia".
Lakini mbona akaamua kuvalia matawi
ya miti?
"Huwa nahisi nina uhusiano wa
karibu na miti, naipenda sana," aliambia.
Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga
picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini.
Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini
kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.
No comments:
Post a Comment