Mwanamume huyo alionekana
akiiharibu nyota hiyo Jumatano jioni.
Waandishi wa habari wanasema
mwanamume huyo alitaka kuipiga mnada kuchangisha pesa za kusaidiwa wanawake
ambao wanadai Bw Trump aliwadhalilisha kimapenzi.
Mgombea huyo amekanusha madai hayo
na kusema ni uongo mtupu.
Mgombea huyo alipewa nyota hiyo mwaka 2007 kutokana na
utangazaji wake katika kipindi cha Apprentice.
Hii si mara ya kwanza kwa nyota
hiyo kuharibiwa.
Miezi michache iliyopita, ukuta wa
mfano uliwekwa kuzunguka nyota hiyo baada yake kutangaza kwamba angejenga ukuta
mpakani wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji wasiingie Marekani.
No comments:
Post a Comment