Maafisa wanasema amekamatwa kwa
kuwa na nyaraka bandia za utambulisho.
Sharbat Gula alipata umaarufu mwaka
1985 kutokana na picha hiy aliyopigwa akiwa na umri wa miaka 12.
Macho yake yalikuwa na rangi ya
kijani, jambo lililomfanya kufahamika kwa jina 'Green-eyed Girl'.
Maafisa wanasema alikamatwa na
Idara ya Uchunguzi ya Pakistan (FIA) baada ya uchunguzi wa miaka miwili
Peshawar, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.
Pakistan ilianza kuwasaka watu
wenye vitambulisho bandia majuzi.
Bi Gula aliwasilisha ombi la kutaka
kitambulisho Aprili 2014 akitumia jina Sharbat Bibi.
Iwapo madai hayo yatathibitishwa,
basi atakuwa mmoja wa maelfu ya wakimbizi kutoka Afghanistan ambao wamejaribu
kukwepa mfumo wa usajili wa watu unaotumia kompyuta nchini Pakistan.
Afisa wa Mamlaka ya Taifa ya
Usajili wa Watu (Nadra) amesema maafisa wa FIA pia wanawatafuta wafanyakazi
watatu ambao wanadaiwa kumpa kitambulisho Bi Gula.
Gazeti la Dawn la Pakistan limesema
Bi Gula alipewa vitambulisho pamoja na wanaume wengine wawili waliodai kuwa
wanawe wa kime.
Picha maarufu ya Bi Gula ilipigwa 1984 alipokuwa kambi
ya wakimbizi kaskazini magharibi mwa Pakistan.
Wakati huo wanajeshi wa Muungano wa
Usovieti walikuwa wameingia Afghanistan.
Mwaka 2002, mpiga picha Steve
McCurry alimtafuta na kumpiga picha. Wakati huo alikuwa anaishi kijiji kimoja
Afghanistan akiwa na mumewe na binti zao watatu.
Baada ya kutokea kwa habari za
kukamatwa kwa Bi Gula, Bw McCurry amesema atafanya kila juhudi kumsaidia
kifedha na kisheria.
"Nimejitolea kufanya kila
niwezalo kutoa msaada wa kifedha na kisheria kwake na familia yake,"
aliandika kwenye Instagram.
Takwimu za Umoja wa Mataifa
zinaonyesha Pakistan inatoa hifadhi kwa wakimbizi 1.4 milioni kutoka
Afghanistan ambao wamesajiliwa. Inakadiriwa kwamba wengine milioni moja
wanaishi humo lakini hawajasajiliwa.
No comments:
Post a Comment