Wakati Serikali ikitangaza msako
kwa watu walioghushi vyeti na kutumia majina ya watu wengine, Waziri wa mambo
ya ndani ya Nchi, Mwigilu Nchemba, ameibuka na kutoa ufafanuzi wa utata wa
majina yake.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka
kwa mjadala wa usahihi wa majina yake pamoja na kuhusishwa kughushi vyeti ya
elimu.
Katika andiko lake aliloliweka jana
katika mitandao ya kijamii ambalo baadaye lilithibitishwa na mmoja wa wasaidizi
wake, Mwigulu alisema watu wanaoandika historia yake hawamjui kwani uhalisia
alikuwa akiitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa Lameck si jina la Kinyiramba na
Madelu si jina halisi la baba yake bali la utani.
“Ni vema kuweka rekodi sawa, kwanza
anasema (aliyeandika) nilikuwa naitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck
sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa
ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu. Ndiyo maana hata kwenye ubunge nililiongeza
tu kama a.k.a ili watu, hasa wazee wanifahamu, hili haliko kwenye vyeti.
“Hili la Lameck siyo jina la
Kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati iliyopo Kijiji cha Mukulu,
daktari tunaita hivyo, lakini ni nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina
la kizungu Lameck.
“Mimi nilipelekwa hospitali
nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wa kiume ni Shumbi, ambalo hata
hivyo wanatumia wazee tu, wanaojua Kinyiramba hilo ndio jina la Kinyiramba,” alisema Mwigulu
na kuongeza:
“Mama yangu aliulizwa jina
akanitaja kwa muuguzi (nesi) akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna
lingine, mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja,” alisema.
Alisema suala hilo ni jambo la
kawadai hasa kwa kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi hadi majina
inakuwa si jambo la kujali.
“Hata pale kijijini kuna wengine
waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya
manesi, matabibu kama mimi, majina ya walimu,” alisema.
Akizungumzia maisha yake ya elimu,
alisema aliacha shule kwa mara ya kwanza mwaka 1984 baada ya kuanza na kaka
yake aliyemtaja kwa jina la Jugulu.
Mbunge huyo wa Iramba alisema
kutokana na hali hiyo, baba yao aliwataka wapeane zamu ya kwenda shule hali
iliyomfanya aache shule.
“Mwaka 1985, nikaachia darasa la
tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza
kufa sana, mzee akashauriwa awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda
nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndiyo nikarudi na nikachukua majina ya
daktari.
“Mtu asichanganye kuona ni
udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga
na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu na mpaka
sasa naona ni struggle (kupambana) za mfano, kuwa nilisoma kwa mazingira ya
kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe,” alisema
Mwigulu.
Waziri huyo alisema kwa anayetaka
kuthibitisha maelezo aliyotoa, anaweza kuwauliza aliosoma nao shule ya msingi.
“Comrades kwa mawazo yangu kosa ni
mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya
mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa
hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua
nafasi ya mtu.
“Halafu watu wanasema jina la mtu,
labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana
jina la mtu, yaani atakuwa John wa Biblia, Mohamed wa Quran, litakuwa la babu,
bibi la mganga, daktari, rafiki, kiongozi au hata la tukio.
“Nijuavyo jina unakula kiapo tu
kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya
nakula kiapo na kutangaza katika Gazeti la Serikali na lisipopingwa ndiyo
linakuwa jina langu jipya.
“Hoja ni kama mtu kapora cheti cha
mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But,
things do change pia kutokana na nyakati na mazingira,” alisema
Mwigulu.
No comments:
Post a Comment