Kuna taarifa kuwa vikosi vya
usalama vimepambana na waandamanaji katika miji mbalimbali, huku watu kadhaa
wakijeruhiwa na wengine kuwekwa kizuizini.
maandamano hayo ni ya wito wa
kumtaka Rais Maduro ajiuzulu juu ya kushindwa kwake katika usimamizi wa Uchumi.
Muungano wa upinzani nchini humo
umetoa masaa 12 ya maandamano ya pamoja siku ya ijumaa ili kuongeza shinikizo
kwa Rais huyo kujiuzulu, ambapo wanamshutumu kwa ukiukwaji wa Demokrasia, na
bunge la nchi hiyo linamshutumu kwa kutaka kupanga mapinduzi.
No comments:
Post a Comment