Msanii mkongwe wa muziki TID pamoja na rapa Bill Nas wameingia studio
kuandaa project mpya ambayo bado hawajaweka wazi ni project ya namna gani.
Miezi kadhaa iliyopita, TID alilalamika kuwa Bill ni mtu mwenye
tamaa na asiye na shukrani baada ya kuondoka Radar Entertainment licha ya
kumlea na kumfikisha pahali.
Kwa sasa wawili hao wapo pamoja na wanaonyesha ushirikiano
katika mambo yao ya muziki.
Alhamisi hii Bill Nas alipost picha instagram akiwa na TID na
kuandika:
#inthekitchen with @tidmusic !!
#NENGA #itsbeenawhile Yo! 2ko Around Mazeee
Bill Nas aliwahi kumshirikisha TID kwenye wimbo ‘Ligi Ndogo’
ambao ulifanya vizuri.
No comments:
Post a Comment