Mwanamume huyo aliuawa kwa kupigwa
risasi.
Hakuna afisa yeyote wa ubalozi huo
aliyeathiriwa na kisa hicho.
"Ubalozi utafungwa Oktoba 28.
Huduma zote za kibalozi zimesitishwa, lakini huduma za kibalozi za dharura kwa
raia wa Marekani zitaendelea kutolewa," taarifa kwenye tovuti ya ubalozi
huo imesema.
Maafisa wa ubalozi huo wametoa wito
kwa raia na wafanyakazi wake kuwa makini kuhusu usalama wao.
Polisi nchini Kenya wanachunguza
kubaini iwapo mwanamume huyo aliyepigwa risasi alikuwa na washirika, afisa
mmoja mkuu wa polisi Vitalis Otieno aliambia shirika la habari la AFP.
Bw Otieno alisema mwanamume huyo
alimdunga kisu afisa mmoja wa polisi lakini akapigwa risasi na kichwani na
kuuawa na afisa aliyekuwa karibu.
Maafisa watano wa idara ya
uchunguzi wa jinai ya Marekani (FBI) walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye
pamoja na polisi wa Kenya kufanya uchunguzi.
Msemaji wa polisi Kenya George
Kinoti alisema mwanamume huyo wa miaka 24 alikuwa "mhalifu wa kuendesha
shughuli zake kivyake", kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Hata hivyo, alisema uchunguzi
unaendelea.
No comments:
Post a Comment