Wamepambana vikali katika masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa silaha, utoaji mimba na uhamiaji haramu.
Na moja kati ya eneo waliovutana ni
kuhusu uhusiano kati Marekani na Urusi na silaha za nyuklia.
Wakati Donald Trump akionyesha kuna
haja ya uhusiano na Urusi na rais Vladmir Putin, Hillary Clinton anaona Urusi
ni hatari kwa Marekani na hata kutupiana maneno makali.
Kuhusu umiliki wa Silaha mgombea
urais wa Democratic amesisitizia msimamo wake kuhusu sheria kali katika umiliki
wa silaha.
Kwa upande wake Donald Trump
alimshutumu Bibi Clinton kwamba amejinufaisha kwa fedha zisizo halali.
No comments:
Post a Comment