Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la
Amina Hamisi (56) mkazi wa mtaa wa mahina kata ya Butimba Jijini Mwanza,
anashikiliwa na polisi baada ya kumlazimisha mjukuu wake aliyejulikana kwa jina
la Rehema Sadiki mwenye umri wa miaka 7 kula kinyesi.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa
Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Augustino Senga amedai kuwa tukio hilo
limetokea Novemba 11, mwaka huu ambapo mtoto huyo alikwenda chooni kujisaidia
na kushindwa kumwagia maji ili kuondoa kinyesi chake ndipo bibi yake ili
kumuadhibu alimuamuru kula kinyesi hicho kitendo ambacho mtoto huyo
alikitekeleza.
Baada ya tukio hilo kutokea raia
wema walitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kufanikiwa
kumkamata mtuhumiwa huyo.
Kamanda Senga ametoa wito kwa
wakazi wa jiii la Mwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudhibiti
vitendo vya kikatili hasa kwa watoto wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni kosa
kisheria hivyo wananchi waache kufanya vitendo hivyo na watakao bainika sheria
itachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment