Siku chache tu baada ya kumpigia debe rais mteule wa Marekani, Donald
Trump — na saa chache baada ya kukatisha njiani show yake ya Sacramento — Kanye
West ameisitisha show yake ya L.A.
Show
hiyo ya Jumapili, ilisitishwa walau saa tatu kabla ya kufanyika. Hadi sasa
hakuna maelezo yaliyotolewa kutoka kwenye label ya Kanye wala promota wa show,
Live Nation kuhusu sababu ya kufanyika hivyo.
Mashabiki waliokuwa wamenununua
tiketi watarudishiwa fedha zao.
Kusitishwa kwa show hiyo kumekuja
wakati ambapo Kanye ameingia kwenye headline kwa kuwadiss Jay Z na Beyonce.
No comments:
Post a Comment