Msanii wa muziki wa
Kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda anajipanga kuachia wimbo mpya ambao
atafunga nao mwaka 2016.
Muimbaji huyo ambaye
anafanya vizuri na wimbo ‘Waache Waoane’ aliomshirikisha Diamond, amesema
muziki umebadilika hivyo msanii hatakiwi kukaa muda mrefu bila kuachia wimbo.
“Kwangu mimi nasema bado mwaka haujaisha kwa sababu muziki
umebadilika sana, msanii anatakiwa asikae muda mrefu bila kuachia wimbo,
binafsi sina muda wakupumzika ni ngoma baada ya ngoma. Kwa hiyo kabla ya mwaka
kuisha nitaachia wimbo mwingine mpya,” alisema Chege.
“Kwa hiyo mashabiki wangu wajue Chege bado nakuja tena waandae
tu masikio yao kwa sasa nipo studio katika maandalizi ya mwisho ya wimbo mpya
ambao utatoka baada tu ya kukamilika,”
Chege ni mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri katika tamasta
la fiesta lililofanya weekend iliyopita katika viwanja vya Leaders Club jijini
Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment