Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi
amesheherekea tukio jingine la kihistoria baada ya kuifungia klabu yake bao
lake la 500 siku ya Jumapili.
Messi
ambaye saivi ana umri wa miaka 29 aliifungia Barcelona bao la kwanza katika
ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla.
Messi ameifungia Barca mabao 500
katika mechi 592,ikiwemo mechi za kirafiki huku mechi 469 zikiwa rasmi.
Messi sasa anakuwa amemshinda
aliyekuwa na mabao mengi Paulino Alcantara ambaye aliichezea Barcelona katika
vipindi viwili vya kati ya 1912 na 1927.
Mnamo mwezi Aprili,mshambuliaji
huyo alifunga bao la 500,ikiwemo mechi za kimataifa,wakati Barcelona
iliposhindwa 2-1 na Valencia.
No comments:
Post a Comment