Dili la Jay Z la kutaka kununua haki miliki ya nyimbo za marehemu Prince
aliyefariki mwezi April, mwaka huu limekataliwa.
Chanzo
kutoka kwenye familia ya marehemu Prince kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa familia
hiyo haina mpango na dili hilo kwa kuwa bosi huyo wa mtandao wa Tidal [Jay Z]
alishawahi kujimilikisha albamu 15 za prince bila ya kibali.
Mwezi uliopita Jay Z aliweka wazi
juu ya kununua haki miliki za nyimbo za Prince ambazo bado hazijatoka kwa
kulipa kiasi cha dola milioni 40 baada ya kufanya mazungumzo na ndugu wa
Prince, Tyka.
No comments:
Post a Comment