Baada ya kuigiza filamu takriban 200, hatimaye Jackie Chan ametunukiwa
tuzo ya heshima ya Oscar.
Muigizaji
huyo wa China alipewa tuzo hiyo Jumamosi kwenye tuzo za Governors.
“After 56 years in the film
industry, making more than 200 films, after so many bones, finally,” alisema
Chan, 62.
Muigizaji huyo alikumbushia kuwa
kuna wakati alikuwa akiangalia tuzo hizo na wazazi wake ambapo baba yake
alimuuliza iweje hajawahi kushinda Oscar licha ya kuwa na filamu kibao.
“I continue to make movies, jumping
through windows, kicking and punching, breaking my bones,” alisema.
Muigizaji huyo alitambulishwa na
staa mwenzake wa filamu ya “Rush Hour” Chris Tucker, muigizaji Michelle Yeoh na
Tom Hanks, ambaye alimuelezea kama “Jackie ‘Chantastic’ Chan.”
Hanks alisema kuwa ni jambo zuri
kutambua kazi za Chan kwa sababu filamu za martial arts na action comedy,
zimekuwa zikitengwa kwenye tuzo.
Muigizaji mkongwe, Arnold
Schwarzenegger amempongeza Chan kwa tuzo hiyo.
Kwenye picha hiyo juu
aliyoiweka Instagram, Schwarzenegger ameandika: Congratulations
to my great friend Jackie Chan on his fantastic honor – after 200 movies, you
certainly deserve this Oscar. You always inspire.
No comments:
Post a Comment