Kwa wanamuziki wa Tanzania, Afrika Kusini imegeuka kuwa kama Kingston,
Jamaica ilivyo kwa wanamuziki wa reggae duniani. SA imekuwa sehemu inayotumiwa
na wasanii wengi wakubwa kufanya video za ngoma zao.
Lakini
huko huko kuna muongozaji aliyeanza kujipatia umaarufu kwa uongozaji wa video
za muziki hususan za hip hop. Jina lake la kazi ni Director Rey.
Nimefanya naye mahojiano ili
kumfahamu zaidi.
Jitambulishe na utuambie umezaliwa wapi?
Jina langu kamili naitwa Ramadhani
Said, mtoto wa kwanza wa kiume kwenye familia ya watoto 4. Nimezaliwa Tanzania,
Dar es – Salaam wilaya ya Temeke. Nimelelewa na wazazi wote wawili mpaka elimu
ya kidato cha 4 ambapo nilikataa kuendelea shule na kuanza kusomea colorist
& computer engineer ndani ya South AAfrica kwa miaka 3. Miaka sita ya kukaa
nje ya nchi imenifanya nikaze jembe kufikia kile ninachotamani.
Kwa sasa wengi wananifahamu kama
“Director Rey” mshindi wa tuzo za 2015 Architect SA Film awards. Colorist I
Visual storyteller na Photographer pia.
Nilikuwa mwanafunzi Cape Town, chuo cha Sanaa, Cape Town Creative
Academ, nimemaliza 2014, nikafanya kazi pale UKZN TV mwaka mmoja, nikaacha na
kuanza focus kwenye TV commercials, music videos & films. Kazi ya picha
sikusomea hata kidogo ujuzi mwingi ni wa kutoka internet, ila music videos
baada ya kufanya kazi na professional director wakati bado nafanya D.O.P tu
wakanishauri nikamate shorty course pale Cape Town kwa miezi 6.
Kazi nyingi nimefanya kama DOP za wasanii wakubwa kabisa SA. Nimefanya
pia na Masandi toka Cashtime LIFE. Na kwa sasa nimeshoot wimbo unaitwa BEEN
THINKIN ni wimbo ambao uko juu sana now radio zote, blogs. Clubs wanaipa sifa,
so nimeshoot hiyo ntaiachia premier kwenye matv na kwenye YouTube channel yangu.
Yes, wapo kama zaidi ya 4 ila nimeshafanya na Shilole – Say My Name.
Nilipata kuonana na Shilole muda mfupi so nikafanya naye video. Mwingine
anaitwa Mauzo – Dear God.
Miaka
6 ya nje ya nchi imenifanya nione thamani kubwa sana nikiangalia Tanzania ya
sasa. Kwa sasa nina kiu ya kushoot ndani ya nchi yangu. Nataka kuwafanya
wasanii wa nchi au ndani ya Africa kuja video zao kushoot Tanzania hiyo ndio
plan.
Video zinafanyika Tanzania zina kasoro gani?
Kasoro zipo, mengi tu ila nafikiri
muda unavyoenda tutajifunza vyema, kwa mfano mavazi ya asili, Tanzania
hatutambuliki vazi letu la hasiri ni lipi… unaimba Kiswahili mavazi ya
Nigerian, video nyingi tu ziko hivyo.
Ni mazingira gani yanafanya kufanya video SA yawe rahisi kwa
msanii?
Ukijulikana na watu basi ni rahisi
kupata chochote, kwa mfano mimi nikitaka gari watanipa kwa sababu profile yangu
inaonekana na kazi wanaziona kwenye matv na internet, so ni mtu ambaye wanajua
nafanya nini. Kingine wenyewe wanasapoti sana entertainment.
No comments:
Post a Comment