Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias aka MC Pilipili amedai
anasumbuliwa na familia yake kuhusu suala la kuoa.
Akiongea
Jumamosi hii, MC pilipili amesema kwa sasa anajipanga kuingia kwenye maisha ya
ndoa baada ya kumpata mtu sahihi ambaye anaweza kumuoa.
“Hivi karibuni Mama yangu alikuwa
anahojiwa pamoja na wadogo zangu wote wakaulizwa ni kitu gani kinawakera kutoka
kwa MC pilipili wakasema hataki kuoa,” alisema MC Pilipili. “Lakini mimi sisemi
nataka kuoa kwa sababu ya kushinikizwa, lakini mambo yakikaa sawa nitaoa kwa
sababu nina msichana nzuri sana,”
Pia mchekeshaji huyo amesema
anaendelea na ziaya yake ya kuandaa matamasha ya kuchekesha mikoani ambapo safari
hii anajipanga kufanya tamasha kubwa Dodoma.
No comments:
Post a Comment