Mmoja kati ya viongozi wa juu wa Tip Top Connection, Madee amedai rapa
Dogo Janja bado hajakuwa kwa kuweza kujisimamia katika muziki wake.
Madee
amesema rapa huyo hawezi kuondoka Tip Top Connection bila ruhusa ya uongozi
wake kwa kuwa tayari alisharubuniwa na akaona madhara yake.
“Wao ambao wanataka kufanya
biashara na Dogo Janja kabla ya kuongea na Dogo Janja basi waufuate uongozi wa
Tip Top hasahasa Madee lakini sio yeye juu kwa juu kwa sababu mimi siamini kama
Dogo Janja anaijua biashara yake kwa sasa hivi,” Madee aliambia 255 ya Clouds
FM.
Aliongeza, “Mimi bado namuona Dogo
Janja bado ni mtoto, hawezi kurubuniwa ndio maana mwanzo alivyorubuniwa na wale
ambao walimrubuni walifanikiwa lakini mwisho wa siku Dogo Janja aliona madhara
yake. So sidhani kama atakuwa na akili za kijinga jinga kama mwanzo za kukurupuka,”
Dogo Janja kwa sasa anafanya vizuri
na wimbo Kidebe.
No comments:
Post a Comment