Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate anataka
kujua hatma yake katika kipindi cha mwezi mmoja iwapo shirikisho la soka nchini
Uingereza FA litamuajiri kama kocha.
Mechi
yake ya mwisho kocha huyo itakuwa ni ya kirafiki itakayochezwa leo 15 November
dhidi ya Uhispania katika uwanja wa Wembley.
Kamati ya FA itaamua ni nani
atakayepewa kazi hiyo,huku Southgate akipigiwa upatu kuchukua wadhfa huo.
”Itakuwa muhimu kwangu mimi kujua
ni nini nitakachofanya baada ya katikati ya mwezi Novemba ”,alisema.
No comments:
Post a Comment