Rais mteule wa Marekani, bilionea
Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa
madarakani.
Trump ameweka msimamo huo jana
katika mahojiano maalum na mtangazaji maarufu, Lesley Stahl katika kipindi cha
60 Minutes, aliyetaka kufahamu kuhusu uamuzi wake juu ya mshahara wake akiwa ni
mfanyabiashara mkubwa.
“Sijawahi kuzungumzia hili, lakini
jibu langu ni hapana,” alisema. “Nafikiri inanibidi kupokea kwa mujibu wa
sheria $1, kwahiyo ntachukua $1 (Sawa na shilingi 2,200 za Tanzania) kwa mwaka.
Lakini hata sijui ni nini,” aliongeza.
Ingawa mtangazaji huyo alimkumbusha
Trump kuwa anaiacha $400,000 kwa mwaka, rais huyo mteule alisisitiza,
“sitachukua mshahara. Sitapokea.”
Wakati wa kampeni, Trump aliahidi
kuwa atajiweka kando na biashara zake endapo atachaguliwa kuwa Rais wa
Marekani, na kwamba atajikita zaidi katika kutimiza ahadi zake kwa Wamarekani.
Alisema kuwa biashara zake ataziacha mikononi mwa watoto wake.
No comments:
Post a Comment