Hapo zamani, Dully Sykes na TID walikuwa kama paka na panya. Na sasa
Dully ameibuka na kudai umri wake na pia kuwa na majukumu mengi, vilimfanya
asione umuhimu wa kuendelea na tofauti zao.
Alikuwa
akizungumza tofauti zilizopo kati ya Diamond na Alikiba na kudai kuwa ipo siku
wakikua, wataacha.
“Hata mimi pia ilivyofikia kwenye
age moja hivi nilikuwa na matatizo na TID, zamani. Lakini nilipoweza kukua
niliacha hivyo, nilivyoanza kupata majukumu nikasahau kwamba tulikuwa na
matatizo,” Dully alimweleza Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times
FM.
Ugomvi
wa TID na Dully ulitokea mwaka 2002 wakati ambapo wote walikuwa wa moto na
kushindanishwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee walipokuwa wakizindua album
zao.
May 2014, Dully alikumbushia kuwa
alimfunika TID kwenye show hiyo. Kauli hiyo haikumpendeza TID aliyeamua kujibu
kwa kusema: TID unaweza kumfunika mzee Mnyama wewe? Alivaa nguo zake za
Kariakoo, kama mapazia hivi,unafikiri Dully Sykes anaweza akanifunika mimi?
Nimesoma shule za kishua, nimefanya muziki kwa intelligence, hao watu wa
Kariakoo washamba.”
Naye Dully alijibu kauli hiyo ya
TID kupitia XXL ya Clouds FM na kusema: Ngoja nikwambie kitu kimoja TID mimi
nimempita miaka mingi, nimempita kila kitu yeye kanipita kasoma ndio
alichonipita TID. Mimi kipindi hicho ndiye nimemkaribisha kwenye industry ‘mimi
ndio Dully Sykes nipo juu mwaka 2002’, miaka mitatu nyuma mimi ndio nimetoka
TID anatoka ndio nimemkaribisha. Halafu uzinduzi wetu TID alikuwa amelipa kosta
mbili pale Magomeni akawaahidi atawapa hela wakifika pale Diamond round ya pili
hajawapa hela ikabidi wale aliowaleta kwenye kosta mbili wamzomee yeye. Kwahiyo
TID kaamua kuongea uongo. Halafu TID ni mdogo wangu anajua mimi ni kaka yake,
historia ipo na picha ninazo. Mimi ndio nilipendeza kushinda TID. TID alikuja
kama mgambo pale alikuja kama mgambo na nguo za mgambo nikisema mwanajeshi
atakuwa juu kidogo. Mimi na miaka mitatu nyuma TID ndo anatoka 2002 na Zeze.
Rafiki yangu kusoma hujui hata hata picha pia, inaeleweka na inajulikana kijana
wangu mdogo ndio hivyo.”
Hivi karibuni bifu hiyo tena
ilionekana kufufuka baada ya verse za Dully zilizokuwepo kwenye wimbo wa TID,
Confidence alioshirikishwa Joh Makini kuondolewa.
No comments:
Post a Comment