Mwanasoka wa zamani wa Uingereza David Beckham bado anaendelea kuingiza
pesa nyingi licha ya kuwa amestaafu soka amepata zaidi ya Pound milioni 11,
kupitia dili za matangazo tu anazofanya kupitia jina na muonekano wake.
David
Beckham amekuwa akitengeneza pesa nyingi kupitia kampuni yake ya Footwork
Productions na bidha kama whisky na vifaa vya michezo ndio vimempa pesa nyingi
zaidi.
Mwaka 2016 Mwezi wa tatu David
Beckham alitajwa kuwa namba mbili kwenye orodha ya wanamichezo waliostaafu
wanaoingiza pesa nyingi zaidi, namba moja ikishikiliwa na mcheza kikapu maarufu
Michael Jordan, akiwa ametengeneza Pound milioni 69 mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment