Baada ya kiu ya muda mrefu kwa mashabiki wa filamu wa Wema Sepetu
hatimaye mwigizaji huyo amesema filamu yake na mwigizaji wa Nigeria, Van Vicker
‘Day After Death’ itazinduliwa Valentine’s Day.
Malkia
huyo wa filamu ambaye amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia filamu, amesema
tayari filamu hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uzinduzi tu.
“Nina movie yangu mpya na Van
Vicker inakuja na nitaifanyia uzinduzi Valentine’s Day kwa sababu ni movie ya
mapenzi,” Wema aliiambia Clouds TV.
Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya
matamasha mbalimbali ya ‘Usiku wa Vigoma’ ambayo yanaambatana na uzinduzi wa
bidhaa zake mpya.
No comments:
Post a Comment