Mwili wa aliyekuwa spika wa
bunge, Samuel Sitta unatarajia kuwasili nchini siku ya Alhamis ukitokea
nchini Ujerumani ambapo alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa hiyo imetolewa na Gerald
Mongela ambaye ni msemaji wa familia.
Amesema mara baada ya mwili huo
kuwasili nchini utapelekwa nyumbani kwa marehemu Masaki jijini Dar es Salaam na
siku ya Ijumaa shughuli za kuaga zitafanyika katika viwanja vya Karimjee kisha
kupelekwa bungeni mjini Dodoma.
“Mwili wa mpendwa wetu mheshimiwa
Samuel Sitta utawasili na ndege ya Emirates siku ya Alhamis saa tisa na nusu
alasiri na baada ya hapo mwili tutauleta hapa nyumbani kwaajili ya kukaa nao na
kupumzika kusubiri ratiba ya Ijumaa,”alisema Mongela.
Mazishi ya Marehemu Samwel John
Sitta yatafanyika siku ya Jumamosi Urambo mkoani Tabora.
No comments:
Post a Comment