Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imesema
kuwa wanatarajia uwanja huo kupokea ndege kubwa zaidi ya 11 kwa mara moja pindi
ukarabati utakapo kamilika.
Meneja
wa upanuzi wa uwanja huo, Mhandisi Mathew Ndossi amekiambia kituo cha runinga
cha ITV kuwa siku chache zijazo uwanja wa KIA utakuwa ni miongoni mwa viwanja
vikubwa vyenye uwezo wa kupokea abiria wengi na ndege nyingi kubwa hali
itakayofanikisha uwanja huo kuingiza fedha za kigeni
Aidha meneja huyo ameongeza kuwa
uwanja wa KIA utaweza kupokea zaidi ya abilia milioni 1 kwa mwaka na kutua
ndege kubwa kumi na moja kwa wakati mmoja.
Kwa sasa mradi huo unaenda pamoja
na ufungaji wa vifaa vya kisasa ili kudhibiti uhalifu uwanjani hapo.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment