Mchekeshaji na mshindi wa Big Brother 2014 Idris Sultan amedai katika
tasnia ya filamu, mrembo Elizabeth Michael ‘Lulu’ ndiye msichana mwenye sifa ya
kumuoa.
Idris
ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Wema Sepetu na baadae kuachana, ameiambia
255 ya XXL ya Clouds FM kuwa Lulu ndiye msichana ambaye anahisi ametulia.
“Mimi naona Elizabeth Michael
ametulia sana,” alisema Idris. “Ni staa ambaye namuona yuko vizuri, amesimama,
mwenye vigezo vya mwanamke ambaye ametulia, anajiheshimu na vitu kama hivyo.”
Aliongeza,”Lakini mwisho wa siku
sisi ni marafiki, yaani unaweza ukanikuta hapo na Lulu yeye amevaa kibikini
chake na mimi nimevaa kiboksa changu lakini niwashkaji tu,”
Idris ambaye pia ni mtangazaji wa
Choice FM, alifunguka hayo baada ya kuulizwa ni mrembo gani bongomovie ambaye
anamtamani kutoka naye kimapenzi.
No comments:
Post a Comment