Serikali ya Tanzania imesema kwamba
kulingana na takwimu inaonesha kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana nchini
Tanzania umepungua kwa asilimia mbili, kutoka asilimia 13.7 mwaka 2012 mpaka
asilimia 11.7 mwaka huu.
Akizungumza jana bungeni,
mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde,
alisema licha ya kupungua huko kwa ukosefu wa ajira, serikali imeweka mipango
ya kuwawezesha vijana kuwa na wigo mpana wa ajira nchini.
Mhe. Mavunde alisema kuwa kwa
takwimu hizo Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kutoa ajira kwa vijana wengi
zaidi kushinda baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.
No comments:
Post a Comment