Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kikosi cha
kupambana na uhalifu wa kutumia silaha za ujambazi limefanikiwa kuwakamata
wanawake wanne na watoto wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi wakifundishwa
mbinu za uhalifu.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kupatikana kwa
wanawake na watoto hao ni baada ya mzazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Shaban
Abdalla mkazi wa kitunda jijini Dar es salaam kutoa taarifa polisi kuwa watoto
wake wanne wametoroshwa na mtalaka wake aliyejulikana kwa jina la Salma Mohamed
kwahiyo jeshi hilo likafanya msako likafanikiwa kuwakamata watoto na wanawake
hao huku mtoto mmoja akiwa ni wa mzazi huyo.
“Jeshi la polisi kanda maalum
katika oparesheni tunayoendelea nayo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es
salaam na Pwani tumefanikiwa kuwakamata watoto wanne na wanawake wanne ambao
wameachishwa shule mbalimbali na wazazi wao au walezi wao mwingine darasa la
pili, mwingine darasa la tatu kwa hiyo tumewakuta wakiwa kwenye nyumba fulani
hao watoto wametoka maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam lakini
kimsingi wanatueleza ni kwamba wanajifunza mbinu zote wapi ambapo wakimpiga mtu
anakufa na wakikupigia hizo ‘push up’huwezi kuamini ni mtoto wa umri ule,”
alisema Kamanda Sirro.
Kamanda Sirro amesema wakati
wakihojiwa kati ya wanawake hao ambao wamekamatwa amesema baada ya kufikishwa
katika eneo hilo la Vikindu mkoani Pwani walimtaka abadilishe jina lake la
kikristo na aitwe jina la Kiislamu na kumtaka kukaa pale kwaajili ya kuwapikia
watoto hao pasipo mama huyo kujua watoto hao wametoka wapi.
“Mama mmoja ambaye ametolewa Mwanza
alipofika alikuwa anatumia jina la kikristu kwahiyo hawakutaka atumie jina la
kikristu wakataka atumie jina la Kiislamu na kukaa na watoto humo ndani
wanachukuliwa maramoja wanakwenda kufundishwa mambo haya ya kivita,”
Aidha Kamanda Sirro alitoa wito kwa
wazazi na walezi na walezi kuwa “Si busara kwa sisi walezi au wazazi wa hawa
watoto hawa watoto bado wanahitajika ndiyo tunasema taifa la kesho watoto
wapate elimu ya msingi ambayo itasaidia katika maisha yao ya kila
siku,tusiwaingize kwenye elimu ambayo mwisho wa siku sana sana watapoteza
maisha yao kwahiyo hao watoto tupo nao na tutahakikisha kwamba tunawarudisha
kwa wazazi wao”.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment