Katika kusherehekea
Christmas mwaka huu, WCB wanatarajia kufanya show yao ya kwanza wakiwa pamoja,
December 24 iliyopewa jina Wasafi Beach Party jijini Dar es Salaam.
Wasanii wote wa label hiyo
wakiongozwa na Diamond watatumbuiza. Lakini huenda kukawa na ugeni mkubwa wa
staa wa nje na tayari meneja wa Diamond, Sallam ametease jina.
Akiweka picha ya mrembo wa Marekani, Amber Rose, Sallam
ameandika kwenye Instagram, “Wangapi watu wanataka huyu dada ashuke bongo siku
akinukishe watu wale nae Bata???”
Naye Diamond alichombeza
kwenye post yake: Eti Manager @sallam_sk anauliza wangapi wangependa huyu dada
@amberrose siku ashuke Bongo watu wale nae Bata???”
Huenda label hiyo ikawa imepanga kumleta mrembo huyo kuwa host
wa tamasha lenyewe.
Hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa ex huyo wa Wiz Khalifa kuja
Afrika. Mwaka jana alienda Lagos, Nigeria kwa mwaliko wa D’Banj ambako hata
hivyo alikaa jukwaani kwa dakika 7 tu.
No comments:
Post a Comment