Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika
likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo
lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa
Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.
Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni
kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema
migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa
sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.
Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya
Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi
kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.
Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada
waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.
“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa
mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na
la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi
wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.
No comments:
Post a Comment