Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amemuandikia
barua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kulalamikia jeshi la magereza mkoa Dodoma
kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema kuwa amesikitishwa sana na
kitendo hicho kinachodaiwa kuwa ni agizo kutoka uongozi mkuu wa Magereza.
“Leo kuna watu ambao wapo
magerezani wamelipiwa tayari, mimi nimeona nisinyamaze, napaza sauti nataka
Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalo tatizo kwa nini mpango
huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?.
“Nimesha muandikia barua Waziri
Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari
tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya
kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha
zoezi hili” amesema Mrema.
Hata hivyo Mrema alisema mpango huo
ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia serikali gharama za
kuwahudumia wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya
Parole katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment