WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watumie fursa ya uwepo wa umeme wa
uhakika kwa kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa ili waweze kujiongzea kipato.
Ametoa wito huo jana (Jumatano, Novemba 16, 2016)
wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa
mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam uliofanyika
kwenye Ofisi za TANESCO zilizoko Mikocheni jijini humo.
Akizungumza kabla ya kubonyeza
kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema: “Umeme ni
mhimili mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi yoyote ile. Tumepata umeme wa
uhakika, tumieni fursa hii ya uwepo wa umeme wa uhakika kujiongezea kipato.”
“Hivi sasa tumepata umeme wa
uhakika, fanyeni kazi kwa bidii ili mfaidi matunda ya kuwepo kwa umeme huo.
Serikali inategemea kwamba sasa wananchi mtaanzisha na kukuza viwanda vidogo
vidogo na vikubwa, biashara zitapanuka na kilimo bora huko vijijini kitaongezeka,”alisema.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda na moja ya nyenzo kuu ya kuendesha uchumi
wa viwanda kwa tija na ufanisi ni upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika,
na ndiyo maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Serikali imefanya
jitihada kubwa kuhakikisha miundombinu ya umeme inaboreshwa ili kuondoa tatizo
la kukatika kwa umeme.
“Wataalam wamenieleza kuwa mradi
huu ulihusisha ujenzi wa kituo kikubwa cha kupozea umeme cha MVA 100, ujenzi wa
njia za usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 132 katika maeneo mbalimbali
ya Jiji kupitia chini ya ardhi, ujenzi wa njia za usambazaji umeme wa msongo wa
kilovoti 33, pamoja na ujenzi wa ujenzi kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji
umeme (Distribution SCADA System) katika msongo wa kilovoti 33 na 11.”
“Kukamilika kwa mradi huu kunaondoa
adha zilizokuwepo awali kutokana na kukatika umeme mara kwa mara. Jiji la Dar
es Salaam ni kitovu cha shughuli za biashara katika kuleta maendeleo ya Taifa
ambapo upatikanaji wa umeme wa uhakika ni wa lazima,” aliongeza.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu
kuzungumza na hadhira iliyokuwepo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo alisema Wakala wa Jiolojia Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa
Jiolojia wa Finland wanaunda mpango wa pamoja wa kuibua madini ya kisasa ambayo
yanatafutwa zaidi duniani kukidhi mahitaji ya kiteknolojia.
“Hivi sasa madini kama graphite na
lithium yanahitajika zaidi kwenye teknolojia za kisasa kama za utengenezaji wa
simu, tuachane na madini yaliyozoeleka kama vile dhahabu na Tanzanite,” alisisitiza.
Alitumia fursa kuuagiza uongozi wa
TANESCO uhakikishe kuwa hakuna mgao wa umeme nchi nzima kwani Watanzania
wamechoshwa na tabia ya kukatiwa umeme mara kwa mara.
“Ili tujenge nchi ya viwanda, tunahitaji umeme wa uhakika, umeme unaotabirika na zaidi ya yote umeme wa bei nafuu,” alisema huku akishangiliwa.
“Ili tujenge nchi ya viwanda, tunahitaji umeme wa uhakika, umeme unaotabirika na zaidi ya yote umeme wa bei nafuu,” alisema huku akishangiliwa.
Naye Waziri wa Biashara za Nje na
Maendeleo wa Finland, Bw. Kai Mykkanen alisema Serikali yake imedhamini ujenzi
wa mradi huo kwa vile inaamini kuwa umeme wa uhakika ni suluhisho la kuondoa
umaskini kwa hiyo kukamilika kwa mradi huo kutaondoa adha ya kukatika umeme
kila mara.
Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo la nishati ya umeme na nishati
mbadala.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba alisema ujenzi wa mradi huo
umegahirimu sh. bilioni 74.6 ambapo kati ya hizo, sh. bilioni 63.56 zimetolewa
na Serikali ya Finland na sh. bilioni 11.03 zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Alisema kukamilika kwa mradi huo
kumewezesha sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam kuwa na njia za mzunguko
(ring circuit) zinaoingizaa umeme.
“Teknolojia hii iliyotumika itawezesha vituo vya kupozea umeme kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia mojawapo inayopeleka umeme itapata hitilafu,” alisema.
“Teknolojia hii iliyotumika itawezesha vituo vya kupozea umeme kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia mojawapo inayopeleka umeme itapata hitilafu,” alisema.
Naye Meneja wa Kituo cha Kudhibiti
Mifumo ya Usambazaji, Eng. Alex Kalanje alimweleza Waziri Mkuu kwamba kwa
kutumia mifumo ya kisasa ya kompyta, (distribution SCADA SYSTEM) kituo hicho
cha udhibiti wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam
kitawasaidia watoa huduma wao waweze kufuatilia kwa haraka zaidi pale matatizo
yanapotokea.
“Baada ya kukamilika kwa kituo
hiki, lengo letu ni kujenga kituo kama hiki kwenye mjai ya Arusha, Mbeya,
Dodoma na Mwanza,” alisema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Biashara na maendeleo wa
Finland, Kai Mykkanen wakatizama moja ya mitambo ya umeme katika Kituo cha
TANESCO cha Mikocheni kabla ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya
Umeme jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (kushoto) wakitazama mfumo wa usambazaji umeme kabla ya Waziri
Mkuu kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam
kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16,
2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen akizungumza
katika Uzindunduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya umeme katika jiji la
Dar es salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye Kituo cha
TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment