Katika hatua ambayo imewafurahisha mashabiki wengi wa muziki nchini, MTV
EMA wanadaiwa kumpokonya tuzo ya Best African Act na Worldwide Act, Wizkid na
kumpa Alikiba ambaye alistahili kushinda.
Siku
chache zilizopita, kulitokea sintofahamu baada ya Wizkid kutangazwa mshindi
ilhali kwenye website ya tuzo hizo, kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye
aliyeshinda.
Alikiba amethibitisha taarifa hizo
wakati akichat live Jumatano hii kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Amesema baada ya mashabiki wake
kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na
makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali, na
sio Wizkid.
“Sasa ndio nimepata confirmation
kwamba ni kweli tuzo inakuja Tanzania na vile vile mimi siwezi kuzungumzia,
nitasubiri mpaka nizishike,” amesema Kiba.
Muimbaji huyo amedai kuwa habari
hizo amezipokea kwa furaha kubwa na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha
kushinda na kuwa nyuma yake.
Wakati hup huo Kiba amempongeza Wizkid kwa ushindi wa
tuzo nyingine ya Afrima. Kwa upande wa Wizkid, tayari amefuta post zote za
Instagram alizokuwa ameweka kushangilia ushindi huo.
Credit: Alikiba Facebook Page/ Papi Chulo Chuly
No comments:
Post a Comment