Hapo mwanzo, wimbo wa
Mwana FA, Dume Suruali ulikuwa ukiitwa Sitoi Hela.
Akiongea kwenye kipindi cha
Ngaz Kwa Ngaz cha EATV wiki iliyopita, Mwana FA alidai kuwa Sitoi Hela ulikuwa
na maneno makali kiasi ambacho kutokana na kuhofia kuwakera wanawake wengine
alilazimika kubadilisha mistari mingi.
“Kuna kitu kilitokea huko nyuma mtaani, kuna neno ‘unajua bana
sisi staff’ Sisi staff kwa maana ya kwamba unajua staff wale wanapanda kwenye
daladala kwamba ‘mimi staff wa gari gani’ sasa wanakuwa hawalipi. So nikafiria
kwamba staff kwa maana kwamba hatutoi hela,” alisema FA.
“Kwahiyo idea ya kwanza wimbo ulikuwa unaitwa ‘Sitoi Hela’ na
niliurekodi kabisa na wimbo ukawa umekamilika. Baadaye tukaja kufikiria ‘kwamba
hii ngoma kali lakini it’s too harsh. Hii wasichana huko barabarani wanaweza
wakatembea na majivu na masizi wanikamate wanisute na chupa za maji, wanipige.
Kwahiyo how do we do it? Tutengeneze balance, beside si tu wanaume suruali,
kuna watu wanakuwa si tu hawataki kuhonga, wanataka kuhongwa wao,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment