Mwanasiasa wa upizani Samy Badibanga, ametagazwa kuwa waziri
mkuu nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo ,kufuatia makubaliano yaliyokumbwa
na utata kati ya serikali na wapizani kwa kuahirisha uchanguzi wa urais hadi
April 2018.
Uchanguzi
mkuu ulistahili kufanyika mwezi huu ambapo wapiga kura nchini DRC walistahii
kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa
muhula wake wa mwisho.
Makubaliano hayo yameongeza hatamu
ya uongozi kwa Joseph Kabila.
Ni siku tatu tangu waziri mkuu
nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, kujiuzulu na kutoa
fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu
pamoja na bwana Ponyo.
No comments:
Post a Comment