Nick wa Pili amekanusha madai yaliyowahi kutolewa na rapper Lord Eyez
dhidi ya member wengine wa Weusi kuwa wamekuwa wakimminya.
Akizungumza na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Nick ambaye ni msemaji wa
kundi/kampuni hiyo, amesema Lord Eyez bado amepigwa benchi. “Kama umesimamishwa
unawezaje kusema unaminywa? Yaani mwanafunzi kama umepewa suspension utasemaje
tena shule inakuminya wakati wewe uko suspended?” amehoji Nick.
“Kila kitu kinaendeshwa kisheria, kwahiyo unaposema unaminywa kuna watu
wanavunja sheria na yeye anaelewa kabisa kanuni na taratibu za kampuni, hakuna
hata mtu mmoja aliyepo kwenye nafasi ya kuvunja sharia kumkandamiza mtu
mwingine, kitu kama hicho hakiwezekani,” ameongeza rapper huyo.
Akiongea
kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, mwanzoni mwa October, 2016, Lord Eyez
alisema akiwa mmoja wa waasisi wa kampuni hiyo, atakuja kueleza zaidi ya ndani
yanayoendelea. Alidai kuwa makubaliano ya kampuni hiyo ni kuwa member asiyepanda
kutumbuiza hapati mkate wake, na yeye kwakuwa hahusiki sana na show zao amekuwa
akiambulia patupu.
“Kimuziki uhusiano wetu na Weusi
mimi Joh Makini Gnako na Nick wa Pili tupo vizuri ila kwenye maslahi kuna
kuminywa sana,” alisema. Rapper huyo aliyewahi kung’ara enzi za Nako 2 Nako,
alipanda kwenye show ya Fiesta jijini Arusha baada ya kualikwa na Barakah Da
Prince. 4
“Nilipanda na Barakah Da Prince
kwasababu Barakah ndiye aliyeona umuhimu wangu mimi kuwepo Arusha. Alinifata
nikiwa bado sijapokea simu ya mtu yeyote,” alisema.
“Kuna watu waliingilia kati kuweka
zengwe nisitumbuize na Barakah lakini nilifanikisha kwa kishindo.”
December mwaka jana hata hivyo
alipohojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Lord Eyez alikuwa na
hadithi tofauti. Alisema bado yupo fresh na kundi hilo na anatarajia kuachia
ngoma mbili, ‘Hardcore’ na ‘Shida Mpya’ alizomshirikisha member wa kundi hilo G
-Nako.
“Lord Eyez bado nipo na nilikuwa na
napikapika vitu,” alisema. “Juzi kati nilikuwa na G-Nako tukiwakilisha Weusi
kampuni na sasa hivi tayari tumeandaa kazi mbili, moja inaitwa Hardcore na
nyingine Shida Mpya,” aliongeza.
“Kwahiyo nawaambia mashabiki wangu
wakae mk
No comments:
Post a Comment