Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama
Scorpion anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika
na hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya
manispaa ya Ilala.
Njwete
anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza kufutwa ambapo
itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada ya kufunguliwa mashtaka mapya.
Huyu ndiye Scropion, kijana
aliyejizolea umaarufu ambapo watu wengi hupenda kumshuhudia kila aingiapo na
kutoka mahakamani huku kila mmoja akizungumza lake kwa kesi inayomkabili.
Alipoingia mahakamani leo, aliomba
ufafanuzi wa wazi juu ya mashtaka yanayomkabili ambapo upande wa jamhuri
kupitia kwa wakili wake Chesensi Gavyole walisema ushahidi umekamilika.
Kutokana na kuombwa ufafanuzi,
Hakimu anayesimamia kesi hiyo Flora Haule amesema baada ya upelelezi huo
kukamilika kesi hiyo itasomwa Novemba 30 mwaka huu, hivyo mshtakiwa atapata
ufafanuzi wa mashtaka yake .
Ikumbukwe kwamba Oktoba 19 mwaka
huu, Salum Njwete maarufu kama Scropion alifutiwa kesi na kisha kusomewa upya
mashtaka yake kutokana na uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliyeomba
kufanya hivyo baada ya hati ya awali kuwa na mapungufu ya kisheria
No comments:
Post a Comment