Nuh Mziwanda amedai kuwa hamhusishi mke wake na kazi yake ya muziki.
Amedai
kuwa mashabiki wake wanaweza kuwa wanamuona kwa nadra jukwaani kwakuwa
hatopenda kumhusisha kwenye muziki.
“Yule hahusiani kabisa na masuala
ya entertainment, yule ni mke wangu mimi, kwahiyo hahusiani na kazi yangu,”
muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Supa Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na
Prince Ramalove.
“Watakuwa wanamuona mara moja moja
lakini yeye na huu muziki wangu ni vitu viwili tofauti,” ameongeza.
Tayari mke wake anatarajia mtoto
wake wa kwanza na muimbaji huyo. Wawili hao walifunga ndoa wiki kadhaa
zilizopita.
No comments:
Post a Comment