Baada ya kuisubiri kwa muda mrefu hatimaye siku rasmi itakayotoka filamu
yas maisha ya Tupac Shakur ‘All Eyez On Me’ imetajwa.
Filamu
hiyo imepangwa kuachiwa siku aliyozaliwa rapper huyo Juni 16, 2017. Kwenye
filamu hiyo Demetrius Shipp ameigiza kama Tupac huku Danai Gurira akiigiza
nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki
mwezi Mei, mwaka huu kwa tatizo la mshtuko wa moyo.
Wakati huo huo Jamal Woolard
ameigiza kama The Notorious B.I.G, Dominic L. Santana ameigiza kama Suge
Knight.
Tupac alifariki dunia Septemba 13,
1996 kwa kupigwa risasi.
No comments:
Post a Comment