Ravi Babu amesema kuwa nguruwe huyo
atashiriki katika filamu yake mpya kwa jina Adhigo ikimaanisha kutoka Telugo
hadi ''there''.
Milolongo mirefu ya benki imekuwa
kitu cha kawaida baada ya noti za rupee za 500 na 1000 kupigwa marufuku nchini
humo katika vita dhidi ya ufisadi.
''Nilikuwa nikimpeleka ili kupigwa
picha nilipogundua kwamba sina fedha za mafuta'',Babu aliambia BBC.
''Nilisimama katika eneo la ATM lakini nikalazimika
kumbeba mimi mwenyewe baada ya kupiga kelele wakati msaidizi wangu alipojaribu
kumbeba.Lazima umbebe ikiwa mkono wako uko katika kifua chake na umuweka karibu
nawe ili ajihisi vyema''.
Picha hiyo imesambazwa katika
mitandao ya kijamii nchini India.
kumekuwepo na visa vya ghasia
nchini India tangu marufuku hiyo ya noti itangazwe ikiwa ni miongoni mwa harakati
za kukabiliana na ufisadi wiki mbili zilizopita.
Watu wamekuwa wakipiga foleni kwa
saa kadhaa nje ya benki pamoja na mashine za ATM ambazo huenda zikaishiwa na
fedha.
Hatua hiyo imeathiri uchumi wa
India.
No comments:
Post a Comment