Hatua ya kwanza ya maandalizi ya
ujenzi wa reli ya Standard Gauge imeshaanza ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi
huo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza itaanza rasmi Disemba 6, 2016.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO) Masanja Kadogosa amesema
serikali imetenga trilioni 1 kwa ajili ya ujenzi huo.
“Ujenzi wa reli ya standard gauge
umeshaanza lakini hatua iliyokuwepo haionekani, tenda zimeshaanza kutangazwa,” alisema
Kadogosa wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini
Dar es Salaam.
Alisema ujenzi huo utaanza kwa
awamu na kwamba awamu ya kwanza inatarajiwa kuanzwa Disemba 6, 2016 wakati ya
pili itaanza Februari 15, 2016.
“Ujenzi huo utachukua miaka mitatu
kukamlika, ambapo utaleta manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho. Pia
utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutokana na kwamba litakuwa na mabehewa
yenye kilomita 2 ambayo sawa na ukubwa wa maroli 300,” alisema.
Alisema wamiliki wa majengo
yatakayo athiriwa na ujenzi huo watalipwa fidia.
“Hifadhi ya reli ina maana kwamba
kila upande inaachwa mita 30, hivyo kama kuna nyumba zitakazokuwa nje ya mita
hizo zitatakiwa kubolewa wamiliki watalipwa fidia,” alisema.
Aidha, Kadogosa alisema kuna miradi
mingine midogo ya ujenzi na ukarabati itafanyika ikiwemo ya ujenzi wa reli mpya
ya Dar es Salaam ambayo itatumiwa kwa ajili ya usafiri kwa wakazi wa jiji hilo.
“Kuna Mradi wa kujenga reli mpya
katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kwa ajili ya treni za abiria ili
kupunguza msongamano wa abiria na magari. Mradi huu uko katika hatua ya
upembuzi yakinifu na usanifu wa awali chini ya kampuni ya ushauri ya GIBB
Engineering ya Afrika Kusini na kwamba inatarajiwa kukamilika Disemba 2016,” alisema.
No comments:
Post a Comment