Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzaia, Job Ndugai (Mb) anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Hafidh Ali Tahir amefariki dunia leo saa 9
alfajiri katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu
zitatolewa hapo baadae. Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba
huu.
Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu
wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa
pamoja na Wabunge katika vikao mpaka saa 2.45 usiku.
No comments:
Post a Comment