Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali
inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama
hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa
ajira nyingi kwa watanzania.
Samia ametoa kauli
hiyo jana Jijini Arusha baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza
mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili kujua changamoto zinazokikabili
kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye
uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Alisema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda
hazina uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka
utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero
kwenye viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru
Millers Atul Mittal alisema kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi
wanazotozwa kwenye viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu
uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania.
Alisema kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10
barani Afrika na kwa Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao
wanafanyakazi katika maeneo mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment